Hatua za kuomba kibali cha Kampuni binafsi ya ulinzi
1. Tengeneza akaunti ya kampuni tarajiwa kwenye mfumo. (majina matatu ya mkurugenzi mmojawapo na
namba yake ya simu inayotumika). na ndiyo itakayo kuwezesha kupata namba ya utambuzi za kuingia kwenye mfumo
TUNZA NAMBA YA UTAMBUZI UTAYOTUMIWA ndiyo itakayotumika kuingia kwenye mfumo kwa awamu nyingine
2. Baada ya kusajili/kuingia(login) utakutana na ukurasa ndani ya ukurasa huo kuna kitufe(request permit) itakayo
kutaka ujaze taarifa kama itakavyoelezwa bila kusahau viamabata/nyaraka tatu kama maelezo hapo chini
3. Utatakiwa kuingia kwa mfumo mara kwa mara kujua mwenendo wa maombi yako ya kibali
Vigezo vya kusajili kibali cha Kampuni binafsi ya ulinzi
1. Kampuni tarajiwa inatakiwa kuwa na wakurugenzi wasiopungua wawili
2. Kampuni tarajiwa inatakiwa kuwa na Mkataba wa makubaliano
3. Wakurugenzi wote wawe na cheti cha hati ya tabia njema
4. Taarifa ya benki ya wakurugenzi
Nyaraka za kuambatisha
1. Mkataba wa makubaliano
2. Hati ya tabia njema
3. Taarifa ya benki
4. Wasifu wa wakurugenzi (cv)